WAHAMASISHENI WADAU WENU KUTUMIA MFUMO WA e-MREJESHO KUWASILISHA KERO ZAO: e-GA

Taasisi za umma nchini, zimetakiwa kuwahimiza wadau wake kutumia mfumo wa e-Mrejesho kuwasilisha kero na maoni mbalimbali sambamba na taasisi hizo kuhakikisha zinashughulikia maoni na kero hizo kwa wakati, kupitia mfumo wa e-Mrejesho ili kuendelea kujenga imani kwa wadau wake.Wito huo umetolewa na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Bi. Subira Kaswaga, wakati wa Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama ‘Sabasaba’...