MAZINGIRA WEZESHI YATAJWA KUCHOCHEA UKUAJI WA SERIKALI MTANDAO

Uwekezaji katika rasilimali watu, miundombinu, fedha, sera na sheria ya Serikali Mtandao umetajwa kuwa kichocheo katika jitihada za ujenzi wa Serikali Mtandao na kurahisisha utendaji kazi Serikalini pamoja na utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi. Hayo yamebainishwa jana (09/09/2024) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba, wakati akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa jitihada za Serikali Mtandao kwe...