FAHAMU MAKOSA SABA (7) AMBAYO MTUMISHI WA UMMA ANAPASWA KUYAEPUKA KATIKA MATUMIZI YA SERIKALI MTANDAO

Serikali Mtandao ni matumizi ya TEHAMA katika utendaji wa kazi Serikalini na utoaji wa huduma kwa wananchi, dhamira kuu ya Serikali Mtandao ni kuongeza ufanisi wa utendaji kazi Serikalini na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kwa urahisi na haraka zaidi mahali walipo. Ili kuhakikisha dhamira ya ujenzi sahihi wa Serikali Mtandao inafikiwa, Sheria ya Serikali Mtandao Na. 10, Sura Na. 273 ya Mwaka 2019, inatoa muongozo wa namna bora ya mat...







