USHIRIKISHWAJI WA WATU WENYE ULEMAVU WACHANGIA UBORESHAJI WA HUDUMA JUMUISHI

Ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika makongamano na mikutano ya kitaaluma, umetajwa kuwa chachu ya uboreshaji wa huduma jumuishi kwa makundi maalumu.Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani Bw. Suleiman Zalala, alipotoa salamu za shukurani wakati wa kilele cha Kikao Kazi cha Nne cha Serikali Mtandao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) uliopo jijin...