MFUMO WA GISP WASAIDIA KUONGEZA UFANISI WA MIRADI YA TEHAMA SERIKALINI

Uwasilishaji wa miradi ya TEHAMA Serikalini katika Tovuti ya Huduma za TEHAMA Serikalini (GISP), umetajwa kuongeza ufanisi wa miradi hiyo kutokana na kutolewa ushauri wa kitaalamu katika hatua za awali unaofanywa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), kabla ya utekelezaji wa miradi hiyo.Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Meneja wa Usimamizi wa Miradi ya TEHAMA kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Bw.Godfrey Masanja, wakati alipofanya maho...