ZUHURA MWINDI: MFANYAKAZI BORA WA e-GA MWAKA 2024

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), imemtangaza Msaidizi wa Mtendaji Mkuu Bi. Zuhura Mwindi, kuwa mfanyakazi bora wa Mamlaka kwa mwaka 2024, baada ya kuibuka mshindi kwa kupata kura nyingi dhidi ya washindani wengine.Uchaguzi wa mfanyakazi bora wa Mamlaka ulifanyika April 25 mwaka huu, baada ya kuwashindanisha wafanyakazi bora 10 kutoka katika Idara na vitengo na kisha Menejimenti kupiga kura ili kumpata mfanyakazi bora wa Mamlaka kwa mwaka wa fe...







