WAZIRI SIMBACHAWENE AWAPONGEZA WANAFUNZI WABUNIFU SEKTA YA TEHAMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. George Simbachawene, amewapongeza wanafunzi wa Vyuo Vikuu wanaoshiriki programu maalum ya mafunzo kwa vitendo inayotolewa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), kwa kubuni mifumo mbalimbali ya TEHAMA, inayosaidia kuongeza ufanisi wa utendaji kazi Serikalini. Mhe. Simbachawene alitoa pongezi hizo Septemba 18, wakati alipofanya ziara ya kikazi katika Kituo cha Utaf...







