NAIBU WAZIRI UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA ANENA FAIDA ZA MFUMO WA MUVU

Naibu Waziri Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe, amesema Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU) utasaidia kutatua changamoto mbalimbali zilikokuwa zikivikabili vyama vya ushirika nchini.Mhe.Kigae alitoa kauli hiyo juzi, wakati wa uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya siku ya Ushirika Duniani yanayofanyika katika viwanja vya Nanenane Ipuli Mkoani Tabora.Alisema, kumekuwa na changamoto mbalimbali katika uendeshaj...







