WIZARA YA AFYA KUENDELEZA USHIRIKIANO NA e-GA

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt.Seif Shekalaghe, amesema kuwa Wizara hiyo itaendelea kuimarisha ushirikiano na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), ili kuhakikisha mifumo yote ya TEHAMA ya kutolea huduma za afya inakidhi matakwa ya Sheria na viwango vya Serikali Mtandao. Dkt. Seif alitoa kauli hiyo juzi jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Umahiri katika masuala ya afya ya Kidigitali (CDH), ambacho kinalenga kuhakikisha utoaji wa hudum...







