MIRADI YA TEHAMA IWASILISHWE e-GA

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), imezitaka taasisi za umma kuhakikisha kuwa miradi na mifumo yote ya TEHAMA inayotekelezwa ndani ya taasisi zao inawasilishwa e-GA wakati wa hatua ya mipango ili kuiwezesha Mamlaka kupitia na kutoa ushauri wa kitaalamu kabla ya utekelezaji wa miradi hiyo. Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja wa Usimamizi wa Udhibiti na Viwango vya Serikali Mtandao Bi. Sultana Seiff, wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili kwa M...







