UJAZAJI NA UTENGENEZAJI WA DODOSO SASA NI KIDIJITALI

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) imefanikiwa kutengeneza mfumo shirikishi wa kidijitali wenye usalama na gharama nafuu unaomuwezesha mwananchi au taasisi kutengeneza na kujaza dodoso, kupata tathmini pamoja na takwimu za dodoso kwa njia ya mtandao. Hayo yalibainishwa na Meneja wa Kituo cha Utafiti na Ubunifu na Uendelezaji wa Serikali Mtandao (eGovRIDC) cha e-GA, Mhandisi Dkt. Jaha Mvulla alipofanya mazungumzo na mwandishi wetu ofisini kwake...







