WATUMISHI WA e-GA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA RUSHWA

Afisa Uchunguzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bi. Dorothea Mrema, amewataka watumishi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kuzingadia uadilifu na weledi katika utekelezaji wa majukumu yao ili kujiepusha na vitendo vya rushwa.Bi Dorothea alitoa kauli hiyo Januari 6 mwaka huu, wakati akitoa elimu kuhusu rushwa mahala pa kazi kwa watumishi wa e-GA, kwenye mkutano wa watumishi hao uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho...