MAAFISA HABARI WATAKIWA KULINDA TAARIFA ZA SERIKALI

Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano wa Serikali, wametakiwa kutumia mifumo rasmi ya Serikali katika mawasiliano ya kikazi ili kulinda taarifa za Serikali dhidi ya vitendo vya uhalifu mtandaoni. Wito huo umetolewa April mwaka huu na Mkurugenzi wa Huduma za TEHAMA wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Bw. Ricco Boma, wakati akichangia mada kuhusu mabadiliko ya teknolojia katika mawasiliano, kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Maa...







