KAMATI YA UFUNDI YA SERIKALI MTANDAO YAFANYA KIKAO CHA KWANZA JIJINI DODOMA

Kamati ya ufundi ya serikali mtandao imefanya kikao cha kwanza na kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na namna ya utekelezaji wa majukumu yake, ili kuhakikisha jitihada za serikali mtandao zinaimarika na kuleta tija kwa Umma. Kikao hicho kilifanyika jana, katika Ofisi za Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) jijini Dodoma, na kuongozwa na Kaimu Mwenyekiti Bw. Eric Kitali Mkurugenzi wa TEHAMA, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mit...







