WAZIRI MHAGAMA AIPONGEZA e-GA KWA UJENZI WA MIFUMO YA TEHAMA KATIKA TAASISI ZA UMMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama (Mb) ameipongeza Mamlaka ya Serikali Mtandao kwa kuziwezesha Taasisi za Umma kutumia Mifumo ya TEHAMA ambayo imesaidia kuboresha utendaji kazi ndani ya Taasisi hizo pamoja na utoaji wa huduma kwa wananchi.Waziri Mhagama aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa uzinduzi rasmi wa Mfumo wa Usimamizi wa Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja - (Collective Investmen...







