WENYE UHITAJI MAALUM KUNUFAIKA NA SERIKALI MTANDAO

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), imeahidi kuendelea kubuni na kuboresha mifumo mbalimbali ya TEHAMA, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za Serikali Mtandao kwa watu wenye mahitaji maalum.Akizungumza katika Maadhimisho ya wiki ya Viziwi duniani 2023, yanayofanyika kitaifa jijini Mbeya, Mkurugenzi wa Huduma na Uwezeshaji e-GA CPA Salum Mussa, amesema sheria ya Serikali Mtandao Namba 10 ya Mwaka 2019, inatambua na kuthamini kundi la watu wenye...