TAASISI ZA UMMA ZAHIMIZWA KUTUMIA GovESB

Kifungu cha 48 (2) cha Sheria ya Serikali Mtandao Na. 10 ya Mwaka 2019, kinaitaka Mamlaka ya Serikali Mtandao kuanzisha na kuendesha Mfumo wa unaowezesha Mifumo ya TEHAMA Serikalini kuwasiliana na kubadilishana taarifa.Katika utekelezaji wa matakwa ya kisheria, e-GA imesanifu, kutengeneza na kusimamia mfumo unaowezesha Mifumo ya serikali kuwasiliana na kubadilishana taarifa unaojulikana kama Government Enterprise Service Bus (GovESB). Mkurugenzi...