WAKAGUZI WA NDANI WATAKIWA KUTOA USHAURI WENYE TIJA KWA SERIKALI KATIKA MIRADI NA MIFUMO YA TEHAMA

Mkaguzi wa Ndani Mkuu Msaidizi, Ofisi ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Bw. Paison Mwamnyasi, amewataka Wakaguzi wa Ndani kuzingatia sheria, kanuni, viwango na miongozo ya Serikali Mtandao wanapofanya ukaguzi kwenye miradi na Mifumo ya TEHAMA, ili waweze kutoa ushauri wenye tija kwa serikali kupitia taarifa zao za ukaguzi. Bw. Mwamnyasi aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya mafunzo maalum kwa Wakaguzi wa Nd...







