TASISI MBALIMBALI ZA UMMA ZAFUNGA HESABU KWA KUTUMIA MFUMO WA ERMS

Tasisi mbalimbali za Umma zimefanikiwa kuandaa na kufunga hesabu kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwa kutumia Mfumo wa kusimamia shughuli na Rasilimali za Tasisi (ERMS).Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja wa Utengenezaji wa Mifumo ya Mamlaka Bw. Donald Samwel wakati wa mahojiano na mwandishi wetu ofisini kwake jijini Dodoma, wakati akieleza mafanikio ya Mfumo wa ERMS kwa mwaka wa fedha 2021/2022.Bw. Donald amezitaja Tasisi hizo kuwa ni Mfuko wa Taifa...







