e-GA yaweka Mikakati Madhubuti ya Kuijenga Serikali Kidijitali

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) itaendele imeweka mikakati madhubuti ya utekelezaji wa jitihada za Serikali Mtandao itakayosaidia kuimarisha na kuijenga serikali kidijitali. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), Mhandisi Benedict Ndomba wakati alipofanya mkutano na waandishi wa habari, kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka. “Katika kipindi cha miaka 10 ijayo, e-GA itaan...







