Wakuu wa Idara/Vitengo Vya TEHAMA Serikalini Wajengewa Uwezo

Taasisi za umma nchini zimetakiwa kuzingatia kikamilifu Sheria ya Serikali Mtandao ya mwaka 2019 na Kanuni zake za mwaka 2020 katika kutekeleza jitihada za Serikali Mtandao mahala pa kazi. Hayo, yameelezwa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, ACP Ibrahim Mahumi kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro wakati akifungua mafunzo kwa Wakuu wa Id...