MATUMIZI YA MIFUMO YA TEHAMA YAMEIMARISHA UWAZI NA UFANISI SERIKALINI.

Mkurugenzi wa Udhibiti na Usalama wa TEHAMA Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Bw. Sylvan Shayo, amesema matumizi ya mifumo ya TEHAMA Serikalini, yameimarisha uwazi na ufanisi kwakuwa, Serikali inao uwezo mkubwa wa kuhifadhi nyaraka, na kupata kumbukumbu kwa usahihi na kwa wakati. Bw.Shayo ameyasema hayo Agosti 26, mwaka huu jijini Dar es Salaam, wakati akiwasilisha mada kuhusu matumizi ya Ofisi Mtandao nda...