UTUMISHI YATEKELEZA MAELEKEZO YA MHE. RAIS KUUNDA MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA WANANCHI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema, ofisi yake kwa kushirikiana na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) imetekeleza maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kusanifu Mfumo wa kielektroniki wa kupokea, kufuatilia na kushughulikia malalamiko (e-Mrejesho) ambao utatoa fursa kwa wananchi na wadau kuwasilisha malalamiko, maoni, mapendekezo, maulizo na pongezi Serikalini.Mhe. J...







