Watumishi na Wananchi kuwasiliana na Waziri Moja kwa Moja

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Mohamed Mchengerwa amezindua mfumo wa kielekroni unaoitwa "Sema na Waziri” Mfumo huu ni maalumu kwa ajili ya kumuwezesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupokea malalamiko, mapendekezo, pongezi au maulizo ya watumishi na wananchi mahali popote na kwa wakati wowote. Akizindua mfumo huo Juni 28, 2021 katika ukumbi wa mik...







