Hudumieni Umma kwa Kuchapisha Taarifa Sahihi: Kalembo

Maafisa Habari Serikalini, wametakiwa kuzingatia weledi katika uandaaji na utoaji wa taarifa za Serikali kupitia tovuti za taasisi, ili kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi kuhusu shughuli na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali kupitia tovuti hizo. Wito huo umetolewa Novemba 18 mwaka huu, na Mkurugenzi wa Huduma za Uwezeshaji wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), Bw. Erick Kalembo, wakati akifungua mafunzo ya Usimamizi na Uen...







