Wadau 1000 wa Serikali Mtandao kukutana Februari Jijini Arusha

Takriban wadau 1000 wa serikali mtandao wanatarajiwa kukutana kwa siku tatu, kuanzia Februari 11 hadi 13, 2025 jijini Arusha, ili kujadiliana kuhusu hali ya utekelezaji wa Serikali Mtandao nchini, kuainisha changamoto, sambamba na kuweka mikakati ya pamoja ya kukabiliana na changamoto hizo. Wadau hao kutoka katika taasisi na mashirika mbalimbali ya umma, wanatarajiwa kukutana katika Mkutano (5) wa mwaka wa Serikali Mtandao, utakaofanyika katik...