e-GA Yawataka Maafisa Waandamizi Kudumisha Uadilifu

Maafisa waandamizi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), wametakiwa kuimarisha waadilifu na kuzingatia vipaumbele vya taasisi na Serikali, ili waweze kuwa viongozi bora wa sasa na baadaye. Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa e-GA, Mhandisi Benedict Ndomba, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uongozi yaliyofanyika hivi karibunimjini Morogoro. Ndomba alisema, mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo Maafisa wakuu na waandamizi wa Mamlaka h...





