WACHAMBUZI WA MIFUMO WAASWA KUONGEZA WELEDI NA UFANISI

Wachambuzi wa Mifumo ya TEHAMA wa taasisi za umma, wameaswa kuongeza weledi na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuepuka makosa yanayoweza kuisababishia hasara serikali. Rai hiyo imetolewa Aprili 18, mwaka huu na Afisa TEHAMA Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Bi. Joan Valentine, wakati wa kuhitimisha mafunzo maalum ya siku tano kwa Wachambuzi wa Mifumo ya TEHAMA (Certified Business Analysis Professional) yaliyofanyika Kib...