emblem

Blogu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma

Huduma za serikali kidigitali

10th Aug 2020

Serikali kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) inafanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa huduma za Serikali zinapatikana kidijitali kwa kutumia mifumo mbalimbali ya TEHAMA.

e-GA ni taasisi ya umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya Serikali Mtandao Na. 10 ya mwaka 2019 kwa lengo la kuratibu, kusimamia na kukuza jitihada za Serikali Mtandao pamoja na kuhimiza utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao kwa taasisi za umma.