emblem

Blogu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma

Kikao Kazi cha Pili cha Serikali Mtandao, 2019

20th Apr 2020

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt. Jabiri Kuwe Bakari akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha Pili cha Serikali Mtandao kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Sayani ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu cha DODOMA (UDOM) Januari 30,2019.

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Kuwe Bakari akisalimiana na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa alipowasili katika Ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano DODOMA kwa ajili ya ufunguzi wa Kikao Kazi cha Pili cha Serikali Mtandao kwa kundi la Makatibu Wakuu na Maofisa Masuuli wa Serikali Kuu na Serikali za Mtaa Februari 1, 2019.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Kuwe Bakari (wa kwanza kushoto) na viongozi wengine Serikalini wakati wa Kikao Kazi cha Pili cha Serikali Mtandao Februari 1, 2019.

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Kuwe Bakari akikabidhi cheti cha ushiriki kwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela Bi.. Sarah Nyagawa, siku ya Utafiti na Ubunifu iliyofanyika Ukumbi wa Chuo Cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu cha DODOMA Februari 2, 2019

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng'i M. Issa akichangia mada wakati wa Kikao Kazi cha Pili cha Serikali Mtandao kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Kompyuta, Habri na Mawasiliano Februari 2, 2019

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Kuwe Bakari alipotembelea banda la Wakala Februari 2, 2019.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akisalimiana na watumishi wa TANAPA alipotembela banda lao wakati wa Kikao Kazi Februari 2, 2019
Maoni