emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Kikao Kazi cha Wakuu wa Idara/Vitengo vya TEHAMA wa Taasisi za Umma

2022-04-28 To 2022-04-29 | Venue | UDOM

Mamlaka ya Serikali Mtandao iliandaa Kikao Kazi kwa ajili ya Wakuu wa Idara/Vitengo vya TEHAMA kutoka Taasisi za Umma kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuanzia tarehe 28 na 29 Aprili, 2022.

Kaulimbiu

Serikali Kidijitali

Angalia Nyaraka Angalia Programu

Wahusika

Kikao Kazi hicho kiliwalenga wakuu wa Idara na Vitengo vya TEHAMA Serikalini na kilihudhuriwa na washiriki wapatao 540

Malengo

Lengo la kikao kazi hicho, lilikua ni kujadili hali ya uzingatiaji wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Serikali Mtandao iliyoidhinishwa wakati wa utekelezaji wa jitihada za Serikali Mtandao katika Taasisi za Umma. Kikao kazi hicho pia kililenga kujenga, kuboresha na kuimarisha uelewa wa pamoja wa masuala ya Serikali Mtandao ili kuhamasisha matumizi bora, sahihi na salama ya TEHAMA na yenye tija katika kuboresha utendaji na kutatua changamoto za utendaji wa Taasisi hizo za Umma.