emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma

Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

 1. Ni lazima usajiliwe kwanza kabla ya kuanza kuingia
 2. Upande wa kushoto chini ya Menyu ya TEHAMA, chagua “Security Incident”
 3. Jaza maeneo yote yanayotakiwa kwa mujibu wa fomu
 4. Bofya kitufe cha “Submit” baada ya kukamilisha
 5. Baada ya kufanikiwa kuwasilisha tukio la usalama, utapokea uthibitisho kuwa umefanikiwa kuwasilisha tukio la usalama
 1. Kama huna akaunti ya huduma kwa mteja, tuma baruapepe kwa egov.helpdesk@ega.go.tz au piga simu +255764292299, +255763292299 kuomba akaunti. Akaunti itafunguliwa kwa watumiaji wa taasisi za umma walioidhinishwa tu. Baruapepe ya kuhakiki itatumwa na kukutaka kutayarisha na kuthibitisha nywila yako
 2. Kama una akaunti ya huduma kwa mteja, tuma baruapepe au piga simu +255764292299, +255763292299 kueleza tatizo unalokabiliana nalo
 1. Ni lazima ulingie/logia kwenye GISP kwa kubofya kitufe cha “login” upande a juu wa ukurasa
 2. Ingiza utambulisho wako (jina la mtumiaji na nywila)
 3. Upande wa kushoto kwenye Menyu ya Huduma, chagua “Requested Services”
 4. Huduma zilizoombwa zitaonekana, halafu tafuta au chagua huduma iliyoombwa kuangalia hatua iliyofikia

Huduma na Mifumo ya Mamlaka imepanwa katika makundi yafuatayo;

 1. Huduma za Ushauri wa Kitaalamu na Msaada wa Kiufundi
 2. Mifumo Shirikishi ya TEHAMA
 3. Huduma ya Kuhifadhi Mifumo (Miundombinu kama Huduma , Mfumo kama Huduma)
 4. Utengenezaji Mfumo
 5. Mtandao wa Mawasiliano Serikalini (GOVNET)
 6. Huduma za Serikali kupitia Simu za Mkononi
 7. Utafiti na Mafunzo
 8. Bango la Matangazo
 1. Lazima uingie/logia kwenye GISP kwa kubofya kitufe cha “login” upande wa juu wa ukurasa
 2. Ingiza utambulisho wako jina la mtumiaji na nywila)
 3. Upande wa kushoto kwenye Menyu ya Mradi wa TEHAMA, chagua “Project List”
 4. Orodha ya Miradi itajitokeza, halafu tafuta au chagua mradi ili uone hatua iliyofikia
 1. Bofya linki ya kuingia/logia upande wa juu wa ukurasa
 2. Ingiza utambulisho wako (jina la mtumiaji na nywila)
 3. Unaweza kupata wasifu wa taasisi yako kwa kubofya kitufe cha “institution profile” upande wa juu wa “tab”. Halafu bofya kitufe cha “edit” kuhariri wasifu wako halafu “ save”
 1. Ni lazima usajiliwe kwanza kabla ya kuanza kuingia/logia
 2. Upande wa kushoto katika Menyu ya TEHAMA, chagua “Register ICT Project”
 3. Jaza maeneo yote yanayotakiwa kwa mujibu wa “Concept Note Form”
 4. Baada ya kukamilisha, bofya “Submit”
 5. Baada ya kufanikiwa kuwasilisha mradi wa TEHAMA uliosajiliwa, utapokea uthibitisho kuwa umefanikiwa kuwasilisha

Nenda kwenye baruapepe yako kuangalia baruapepe ya kufungua ili uweze kutumia akaunti yako. Kama hakuna baruapepe, toa taarifa kupitia dawati la msaada au mratibu wa mafunzo wa e-GA kuweza kutanzua tatizo hilo

Baada ya kusajili akaunti yak tu, utapokea baruapepe yenye linki ya kufungua. Bofya kufungua akaunti yako ya TSMS

Sababu

 1. Tatizo la kuunganishwa na intaneti
 2. Seva haipaikani kwa muda na matatizo ya mtandao yataweza kukatisha utaratibu mzima

Ufumbuzi:

 1. Hakikisha mtandao uko imara
 2. Kama tatizo linaendelea, kwa msaada zaidi wasiliana na msimamizi wa GMS wa taasisi yako

Sababu

 1. Mtandao unashindwa kuunganishwa kwa haraka
 2. Ukubwa wa jalada umzidi kiwango kinachoruhusiwa cha 20MB

Ufumbuzi

Njia ya 1

Kama tatizo linasababishwa na kasi ya uunganishaji;

 1. Thibitisha kama tatizo ni kasi ya mtandao kwa kufungua mitandao mingine kama vile Google, yahoo n.k. Iwapo mitandao hiyo inafunguka kwa urahisi, basi kuna tatizo kwenye mtandao wako, kwa msaada zaidi wasiliana na msimamizi wa GMS wa taasisi yako
 2. Kama mitandao mingine nayo haifunguki, tafuta mtandao wa intanet mbadala wa haraka. Kwa mfano tumia modem
 3. Ambatisha tena jalada na tatizo litakwisha

Njia ya 2

Kama Ukubwa wa jalada umezidi kiwango kinachoruhusiwa;

 1. Kama unatuma majalada mengi, yatume katika vikundi vidogovidogo, tatizo litakwisha
 2. Kama unatuma jalada moja tu linalozidi kiwango kinachoruhusiwa (20 MB), punguza jalada kulingana na ukubwa ulioruhusiwa. Tumia mifumo tumizi ya kupunguzia kama vile WinRAR au ZIP. Kama hauna mifumo hiyo, kwa msaada zaidi wasiliana na msimamizi wa GMS wa taasisi yako
 3. Ukikamilisha njia ya pili hapo juu, ambatisha tena jalada na tatizo litakwisha
 4. Kama tatizo linaendelea, kwa msaada zaidi, wasiliana na msimamizi wa GMS wa taasisi yako

Sababu

 1. Ama unatuma baruapepe kwa kikundi kisichoidhinishwa
 2. Kunatokea alama kama vile -,*,> n.k kwenye uga wa anwani yako (To: Cc: or Bcc :)
 3. Seva ya baruapepe imekataa kuhalalisha mpokeaji mmoja au zaidi

Ufumbuzi

 1. Logua kwa kubofya kitufe cha “logua” na logia tena. Hatua hii itatanzua tatizo lako
 2. .Kama tatizo linaendelea, kwa msaada zaidi wasiliana na msimamizi wa mfumo wa GMS katika taasisi yako.