emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Matumizi ya TEHAMA katika Kuboresha Utendaji Kazi Serikalini


Matumizi ya TEHAMA katika Kuboresha Utendaji Kazi Serikalini


Wakala ya Serikali Mtandao imebuni, imesanifu na imetengeneza mfumo shirikishi wa Kusimamia Shughuli na Rasilimali za Taasisi (ERMS). Mfumo huu unaunganisha shughuli mbalimbali za Taasisi kuwa katika mfumo mmoja unaowezesha usimamizi, ufuatiliaji, ukaguzi na tathimini ya utekelezaji wa shughuli zote za Taasisi kwa ufanisi.

Akifafanua kuhusu mfumo huu, Mtendaji Mkuu wa Wakala Dkt, Jabiri Bakari amesema, “Tumeamua kutumia utajiri wa utaalamu wetu wa kidigitali kutengeneza Mfumo huu (ERMS) ambao ni dirisha moja linalounganisha shughuli zote ndani ya Taasisi ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na utoaji wa huduma bora kwa umma.” Kwa taarifa zaidi, bofya hapa