emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Maadili Wapewa Mafunzo


Maadili Wapewa Mafunzo


Maofisa TEHAMA na Habari wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wamepewa mafunzo ya kupandisha taarifa kwenye Tovuti yao mpya inayopatikana kwa anuani ya www.ethicssecretariet.go.tz.

Ofisa Habari wa Sekretarieti ya Maadili, Bi. Joanither Barango, amesema kuwa tovuti yao ya awali haikuwa rafiki hasa katika uwekaji wa taarifa pia haikuwa na uwezo wa kuwa na taarifa nyingine walizotamani zipatikane kwenye tovuti hiyo.

“Uwekaji taarifa kwenye tovuti yetu ya awali ulikuwa ni mgumu sana  na ilimlazimu mtaalamu wa TEHAMA afanye kazi hiyo, lakini tovuti ya sasa iliyotengenezwa na Wakala ya Serikali Mtandao ni rahisi kuitumia na inawezesha kazi kufanywa na wataalamu wa Habari wenye bila ya kuwategemea wataalamu wa TEHAMA”  alisema Bi. Joanither.

Pia Bi. Joanither aliongezea kwa kusema kuwa tovuti yao ya awali haikuwa na uwezo wa kupandisha video, kwa hiyo mwananchi alikosa fursa ya kuona matukio na shughuli mbalimbali za ofisi hiyo ikiwemo kuapishwa viongozi, lakini tovuti hii mpya ina uwezo wa kuweka video.

Naye Ofisa TEHAMA wa Sekretarieti ya Maadili Bw. Francis Toke amesema kuwa anaishukuru Wakala kwa kuweza kuwatengenezea tovuti nzuri iliyofuata Miongozo yote iliyowekwa na Serikali kupitia Wakala na  itakayosaidia kuiweka taasisi yao  karibu na wananchi wake hasa kwa uwezo wa tovuti hiyo kupokea maoni na malalamiko mbalimbali kutoka kwao na kuyajibu.

Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wa kupandisha taarifa na kuwaongezea ujuzi wa kutumia tovuti kwa Maofisa Habari na TEHAMA wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, yamefanyika katika ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao kuanzia Julai 24 hadi 28, 2017.