emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma

Mitsubishi Pajero 4WD, Station Wagon Kuuzwa kwa Mnada wa Hadhara


Mitsubishi Pajero 4WD, Station Wagon Kuuzwa kwa Mnada wa Hadhara


Wakala ya Serikali Mtandao itauza kwa njia ya mnada wa hadhara gari chakavu aina ya Mitsubishi Pajero 4WD, Station Wagon ikiwa ni 2.8L injini ya Dizeli. Wananchi wote wanakaribishwa kushiriki katika mnada huo utakaofanyika siku ya Ijumaa tarehe 25 Januari, 2019 kuanzia saa nne asubuhi katika eneo la karakana ya Temesa Mt. Depot, Dar es Salaam.

Aidha, kwa yeyote atakayeshiriki mnada huo anaombwa kufika karakana ya Temesa Mt. Depot, Dar es Salaam kukagua gari hilo siku za kazi kasoro jumamosi na jumapili ambapo ukaguzi utaruhusiwa kufanyika kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka saa 10:00 jioni.

Modeli ya gari ni Pajero st Wagon yenye namba ya usajili STL 2628, namba ya Chesesi JMYLNV96WFJ000176 na namba ya injini ni 4M40215HP1015.

Gari hilo litauzwa kama lilivyo mahali lilipo namnunuzi atalazimika kulipa papo hapo amana isiyopungua asilimia Ishirini na Tano (25%) ya thamani ya gari na atakamilisha malipo yote ndani ya muda wa siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya mnada. Mnunuzi akishindwa kutimiza sharti hilo atakosa haki zote za ununuzi wa gari na amana iliyolipwa haitarudishwa.

Vilevile, Mnunuzi atatakiwa kuondosha au kuchukua gari ndani ya muda wa siku saba (07) kuanzia siku ya kukamilisha malipo.