emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma imepata msiba


Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma imepata msiba


Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma imepata msiba wa kuondokewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina O. Kombani (Mb) aliyefariki tarehe 24 Septemba, 2015 katika Hospitali ya Apollo nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na Serikali kwa ujumla kwa kuondokewa na kiongozi mchapakazi, mwadilifu, mzalendo na aliyekuwa na mapenzi mema na nchi yake.

Wakati wa uhai wake, Mhe. Kombani alijitoa kulitumikia taifa bila ubaguzi wala upendeleo wowote, hivyo Ofisi itamuenzi kwa kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali katika Utumishi wa Umma kama alivyokuwa akisisitiza.

Mhe. Kombani aliteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma mwaka 2012 akitokea Wizara ya Katiba na Sheria. Mhe. Kombani amekitumikia cheo hicho mpaka mauti yalipomfika.

Pumzika kwa Amani mpendwa wetu, Ofisi itaendelea kukukumbuka daima kwa busara zako na uongozi wako uliotukuka.