emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Maafisa Habari na Wachambuzi wa Mifumo ya kompyuta


Maafisa Habari na Wachambuzi wa Mifumo ya kompyuta


Wakala ya Serikali Mtandao(eGA) inaendesha mafunzo ya kupandisha taarifa kwenye tovuti kwa taasisi ya Shirika la Elimu Kibaha (Kibaha Education Centre), Halmashauri ya jiji la Dar es salaa (Dar es salaam City Council, Tume ya Utumishi wa Umma (Public Service Commission), Manispaa ya Ilala (Ilala Municipal) na Mamlaka ya Taifa ya Uhifadhi wa Chakula (National Food Reserve Authority).

Mafunzo hayo yameanza tarehe 9 hadi 13 Februari,2015 katika ukumbi wa mafunzo wa Wakala ya Serkaiali Mtandao.Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Maofisa kumi (Mawasiliano na Tehama) taasisi mbalimbali za Serikali.

Wakala ya Serikali Mtandao (e-Government Agency) ni Taasisi ya Serikali iliyoundwa kwa sheria ya Wakala za Serikali Na. 30, Sura ya 245 ya mwaka 1997. Wakala hii ina jukumu na mamlaka ya kuratibu, kusimamia na kukuza jitihada za Serikali Mtandao nchini Tanzania. Wakala imekuwa ikisanifu na kutengeneza tovuti mbalimbali za Serikali ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa Umma.Pia imekuwa ikiendesha mafunzo ili kuwajengea uwezo na ujuzi maafisa hao katika kuandaa, kuhuisha na kupandisha taarifa mbalimbali za taasisi kwa ajili ya tovuti zao.