emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Maafisa Habari na Wachambuzi wa Mifumo ya kompyuta wa Halmashauri za Mkoa wa Morogoro


Maafisa Habari na Wachambuzi wa Mifumo ya kompyuta wa Halmashauri za Mkoa wa Morogoro


Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt. Jabiri Bakari amewataka Maafisa Habari na Wachambuzi wa Mifumo ya kompyuta wa Halmashauri za Mkoa wa Morogoro kutumia ujuzi wao kikamilifu ili kuhakikisha wanatoa taarifa muhimu zinazohusu maswala ya Kijamii kupitia tovuti zao.

Alitoa wito huo Oktoba 20 2014 wakati akifungua warsha ya siku tano ya mafunzo kwa Maafisa Habari na Wataalamu wa Teknolojia ya Kompyuta yaliyofanyika Jijini Dar es salaam katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi za Wakala.

Dkt. Bakari aliwambia wataalamu hao kuhakikisha wanaonyesha huduma muhimu za kijamii pamoja na shughuli nyingine muhimu zinazofanywa katika Halmashauri na Manispaa zao ili kuwawezesha wananchi kupata taarifa muhimu kuhusu serikali inavyotekeleza  majukumu yake.

“Tunatengeneza muonekano wa mbele (Dash Board) wa tovuti mtakazozitengeneza, kwa hiyo kuhakikisheni mnaibua shughuli muhimu zitakazowezesha wananchi kunufaika katika Nyanja zote lakini pia na taasisi zenu ziweze kunufaika kutokana na mapato yatakayopatikana kupitia matangazo madogo madogo ya kibiashara” Alisema Dkt. Bakari.

 

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta kutoka ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Gracian Makota alisema kupitia warsha hiyo wanategemea kuleta mabadiliko makubwa na kuongeza ufanisi katika sekta ya Teknolojia, Habari na Mawasiliano hali itakayoleta chachu ya maendeleo kwenye Halmashauri za Wilaya na Manispaa mkoani humo.