emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Mafunzo ya Usimamizi wa Mfumo wa Barua Pepe Serikalini yatolewa


Mafunzo ya Usimamizi wa Mfumo wa Barua Pepe Serikalini yatolewa


Mkurugenzi wa Usimamizi wa TEHAMA Bw. Benedict Ndomba amewataka watumishi wa Serikali kuhamasisha taasisi zao zitumie Mfumo wa Barua Pepe Serikalini ili kuwa na mawasiliano salama kati ya taasisi za Serikali.

 Aliyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya Matumizi ya mfumo wa Barua Pepe Serikalini (Government Mailing System) kwa taasisi nane (8) za Serikali yaliyofanyika Machi 4, 2015 katika Ofisi ya Wakala. 

“Serikali ilitoa tamko kuwa taasisi zote zitumie mfumo huo na ni vema taasisi hizo zianze matumizi hayo mapema”,alisema Bw. Ndomba.

 Mafunzo hayo ya siku moja yalijumuisha Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa(TAKUKURU), Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), Chuo cha Utalii cha Taifa (NCT), Mkoa wa Dodoma na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na yalihudhuriwa na jumla ya washiriki 11 kutoka kwenye taasisi hizo.

 Wakala imekuwa ikitoa mafunzo mbalimbali ikiwemo Matumizi ya Barua Pepe Serikalini ili kuwajengea uwezo watumishi wa taasisi mbalimbali za umma ili ziweze kuendesha shughuli zake kwa urahisi na kutoa huduma bora kwa wananchi.