emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Taasisi 72 Kupata Mafunzo ya “Cyberoam"


Taasisi  72 Kupata Mafunzo ya “Cyberoam


Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) kupitia Idara ya Mtandao wa Serikali (GovNet) inaendesha mafunzo ya “Cyberome” kwa Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala za Serikali - MDAs 72  kuanzia Machi 9-11 kwa kundi la kwanza na tarehe16-18 Machi, 2015 kwa kundi la pili

 Mafunzo hayo yanayofanyika katika hoteli ya Belinda Oceanic Resort yanahusisha Maofisa TEHAMA (Technical Staff) 72 kutoka taasisi hizo ambapo awamu ya kwanza kutakuwa na washiriki 36 na awamu ya pili ambayo ni ya mwisho itahusisha washiriki 36.

Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Usimamizi wa TEHAMA kutoka Wakala ya Serikali Mtandao Bw. Benedict Ndomba amesema ni kipaumbele cha Wakala kuhakikisha kuwa mawasiliano yote ya Serikali yanakuwa salama.

“Serikali inahitaji mtandao wa mawasiliano uliobora, unaoaminika, unaotegemewa na salama”, alisema Ndomba.

Vilevile Bw. Ndomba amesema Wakala ina wajibu wa kuwajengea uwezo Maofisa TEHAMA na kuhakikisha kuwa kuna matumizi sahihi ya TEHAMA Serikalini.

Aidha Wakala  itaendelea kuandaa mafunzo hayo mara kwa mara ili kutimiza azma iliyojiwekea.

Naye Mkurugenzi wa Uratibu wa Miundombinu ya TEHAMA (DCIO) Bw. Benjamin Dotto amesema lengo la mafunzo ni kuwajengea uwezo Maofisa hao ili kuweza kusaidia katika masuala ya utawala, uendeshaji na matengenezo ya Mtandao Serikalini pamoja na kuwaongezea ujuzi wa kuvimudu vifaa hivyo katika taasisi zao.

Aidha, Meneja wa Kitengo cha Mtandao Serikalini Bw. Ricco Boma amesema washiriki wamefanya mtihani utakaowapatia cheti cha taaluma husika.

“ Mtihani unaofanyika unatungwa na kampuni kubwa duniani iliyojikita katika vifaa vya kompyuta na mtandao inayoitwa Cisco ambapo wanaandaa maswali na kuyatuma kupitia mtandao na mtihani huo ni bure kwa atakayeufanya, na endapo mtu atafeli, anazo nafasi mbili za kurudia”, alisema Boma.

Vilevile Afisa TEHAMA aliyehudhuria mafunzo hayo, Bw. Gilbert Makero amesema mafunzo hayo yana tija kwa taasisi za Serikali kwa kuwa itakuwa rahisi kudhibiti matumizimengine ya mitandao ya kijamii kwa watumishi wa Umma wakiwa ndani ya muda wa kazi.

Wakala ya Serikali Mtandao inaunganisha Taasisi za Umma 72 katika mtandao mmoja wa mawasiliano ambao ni salama na wenye gharama nafuu kwa ajili ya data na mawasiliano na  taasisi zote za umma zitakuwa ndani ya mtandao mmoja wa mawasiliano wa  Serikali (LANs).