emblem

Blogu ya Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma

Taarifa Mpya

Ufunguzi wa mafunzo ya TEHAMA DODOMA

Ufunguzi wa mafunzo ya TEHAMA DODOMA

17th Apr 2020

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) alifungua mafunzo ya TEHAMA kwa maofisa wa serikali katika kituo cha UCC Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo maofisa TEHAMA Serikalini

Kikao Kazi cha Kwanza cha Serikali Mtandao Agosti 17-20, 2015

Kikao Kazi cha Kwanza cha Serikali Mtandao Agosti 17-20, 2015

17th Apr 2020

Wakala ya Serikali Mtandao iliandaa Kikao Kazi cha kwanza cha Serikali Mtandao kilichofanyika Agosti 17-20, 2015 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) Arusha. Kikao Kazi hicho kilihudhuriwa na washiriki 770 kutoka taasisi za umma pamoja na wataalam kutoka nchi a India na Singapore ambazo zinafanya vizuri katika utekelezaji wa Serikali Mtandao

Wiki ya Utumishi wa Umma

Wiki ya Utumishi wa Umma

16th Apr 2020

Wakala imeshiriki kwenye maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika kila mwaka kwa lengo la kujitangaza, kuelimisha na kupata maoni ya umma kwa jumla. Wakala imeshiriki mara kwa mara kwenye maonesho hayo, mwaka 2014 ilishika nafasi ya tisa kwenye kundi la taasisi zenye ubunifu zaidi kati ya taasisi 84 na mwaka 2015 ilishinda nafasi ya nne kati ya taasisi 70 kwenye mashindano ya taasisi zinazosimamiwa vizuri zaidi. Mwaka 2016 Wakala iliadhimisha wiki hiyo kwa kutembelea taasisi 34 na kuzipa msaada wa kiufundi.

Uzinduzi wa Tovuti Kuu ya Serikali Novemba 29, 2013

Uzinduzi wa Tovuti Kuu ya Serikali Novemba 29, 2013

16th Apr 2020

Tovuti Kuu ya Serikali inayopatikana kwa anwani https://www.tanzania.go.tz ilizinduliwa rasmi na aliyekuwa Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda katika ukumbi wa Kituo chaKimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere-Dar es Salaam Novemba 29, 2013

Uzinduzi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Julai 12, 2012

Uzinduzi wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Julai 12, 2012

16th Apr 2020

Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) ilizinduliwa rasmi na aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika ukumbi wa Karimjee , Dar es Salaam Julai 12, 2012