ERMS ni mfumo shirikishi wa kusimamia Shughuli na Rasilimali za Taasisi wenye moduli 20 zinazowasiliana na Kuunganisha Shughuli za Idara na Vitengo ndani na kati ya Taasisi.Tazama moduli hizo zinavyofanya kazi.
Taasisi inaweza kutumia mGov kutuma SMS kwa wadau wake (PUSH SMS), inamwezesha mwananchi kupata huduma mbalimbali kama vile kuulizia bili ya maji (PULL SMS) na pia mGov inatoa huduma ya e-wallet inayomwezesha mwananchi kulipia huduma mbalimbali za kiserikali kupitia wallet akaunti ya mtandao wake wa simu.
"Mfumo huu wa ERMS unatumika kusimamia shughuli za ndani za taasisi kwa kutumia moduli 20 zinazowasiliana na kuunganisha shughuli za Idara na Vitengo", Dkt. Bakari
Kamati za Utekelezaji wa Serikali Mtandao zimeanzishwa ili kuisaidia Mamlaka katika utekelezaji wa Sheria ya Seikali Mtandao ili kuwa na matumizi ya TEHAMA yenye tija
Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) ni taasisi ya umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya Serikali Mtandao Na. 10 ya mwaka 2019. Ni taasisi yenye mamlaka ya kuratibu, kusimamia na kukuza jitihada za Serikali Mtandao pamoja na kuhimiza utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao kwa taasisi za umma